Mfuko wa Afya wa Jumuiya ya SUA (SCHS) ni Mfuko wa Afya wa Jumuiya ya Chuo ulioanzishwa na Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) mwaka 2007 ukiwa na lengo la kuboresha huduma za afya kwenye Jumuiya ya SUA na maeneo yanayozunguka. Kwa sasa Mfuko huu unafanya kazi kama Mfuko wa afya wa ziada (supplementary Scheme) ukichangia huduma za matibabu kwa wanufaika wake kwa ambazo hazitolewi na Bima ya afya ya Taifa, (NHIF)