Faida za Mfuko wa SCHS zinatokana na huduma nyingi nzuri na rafiki zitolewazo kwa Wanufaika wake ikilinganishwa na Mifuko mingine ya aina yake. Zifuatazo ni baadhi ya faida za SCHS dhidi ya Mifuko mingine ya Afya:-
Huduma ya kusafirisha Mgonjwa kutoka mahali alipo hadi hospitali husika (Ambulance);
Huduma zote za matibabu katika Zahanati, kituo cha Afya, Hospitali ya Wilaya, Hospitali za Rufaa za Mkoa na Kitaifa;
Huduma za dawa na vifaa tiba zisizotolewa na Mifuko mingine bila mwanachama kuongeza malipo ya ziada;
Huduma za dawa zenye “brand” pindi Daktari anapoona uhitaji kwa mgonjwa;
Fursa kwa mgonjwa kupata huduma za Matibabu kwa utaratibu maalum na wa haraka;
Kurejesha fedha za matibabu kwa huduma zilizoidhinishwa na Daktari;
Huduma kwa wastaafu wanaoendelea kuchangia asilimia 3 ya pensheni yao kila mwezi pamoja na wenzi wao;
Huduma za matibabu sawa na kila hatua ya huduma Mwanachama anayopitia;
Kuchangia huduma za matibabu ya nje ya nchi pale inaposhindikana katika Hospitali za Rufaa za hapa nchini;
Huduma ya kuchukua dawa kwenye maduka ya madawa ambayo Mfuko umeingia nayo mkataba ili kuhakikisha mwanachama hakosi dawa endapo atakosa dawa katika hospitali husika, na;
Kuchangia huduma hizi hutolewa kwa wanufaika wote yaani wanachama wachangiaji pamoja na wategemezi wao.