Kujiunga na Mfuko huu ni kwa hiari ambapo kwa Wafanyakazi kuchangia 2% ya mshahara wake kwa mwezi na kwa wastaafu kuchangia 3% ya pensheni yake kwa mwezi. Upeo wa huduma za afya kwa Wanachama ni kwa Mwanachama mwenyewe na mwenzi wake pamoja na wategemezi wanne ikijumuisha wazazi na watoto wasiozidi umri wa miaka 25 wa Mwanachama. Kwa wastaafu ni Mwanachama na mwenzi wake.